• HABARI MPYA

    Wednesday, July 22, 2020

    BEN POL ASHlRlKlANA NA 2FACE IDIBIA, YEMI ALADE NA AMANDA BLACK KATIKA WMBO STAND TOGETHER

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSANII wa muziki wa kizazi kimya nchini Benard Paul ‘Ben Pol’, ni miongoni mwa wasanii  10 wa Afrika walioimba kwa pamoja wimbo  maalum wa kujilinda na maambuzi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVlD19.
    Akizungumza na tovuti hii, Ben Pol amesema kwamba wimbo huo unaitwa Stand Together, ambao ameshirikiana na 2face Idibia wa nchini Nigeria), Ahmed Soultan wa Morocco, Teni na Yemi Alade wa Nigeria na Amanda Black  wa Afrika Kusini.
    Ben Pol amesema wasanii wengine alioshirikiana nao n iStanley Enow wa Cameroon, Gigi LaMayane wa Afrika Kusini, Prodigio wa Angola na Betty G wa Ethiopia, lengo likiwani kuhamasisha Afrika nzima kuendelea kujikinga na kutopata maambuziki ya ugonjwa huo ambao umekuwa tishio kila nchini.
    Pol alisema kuna baadhi ya nchini za Afrika zina ukaribu wa kuingia nchi moja baada ya nyingine hata baadhi ya familia kujumuika pamoja, ambapo sasa imekuwa tofauti, ambapo kila mmoja anahitajika kumuelemiusha mwingi ne ili ugonjwa huo uondoke Afrika na dunia kwa ujumla.
    “Tumefanya wimbo huu lengo ni kuhamasisha Afrika nzima, kuendelea kuchukua taadhari , kila mmoja wetu aendelee kuhamasisha ikiwa ni pamoja na kujilinda na kuwalinda wengine, wajiepushe na Corona”alisema Ben Pol.
    Aidha Pol  alisema kuwa kuna baadhi ya nchini barani Afrika bado wana tatizo kubwa na wananchi wake kupatwa na maambuziki ya ugonjjwa huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEN POL ASHlRlKlANA NA 2FACE IDIBIA, YEMI ALADE NA AMANDA BLACK KATIKA WMBO STAND TOGETHER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top