• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 09, 2020

  SALAH APIGA MBILI LIVERPOOL YAICHAPA BRIGHTON 3-1

  Mohamed Salah (wa pili kushoto) akipongezwa na wenzake, Naby Keita (kushoto), Roberto Firmino na Alex Oxlade-Chamberlain baada ya kuifungia Liverpool mabao mawili dakika ya sita na 76 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Brighton & Hove Albion kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Amex. Bao lingine la Liverpool lilifungwa na Jordan Henderson dakika ya nane, wakati bao pekee la Brighton lilifungwa na Leandro Trossard dakika ya 45. Kwa ushindi huo, Liverpool ambao ni mabingwa tayari, wanafikisha pointi 92, sasa wakiwazidi pointi 23 Manchester City wanaofuatia baada ya kucheza mechi 34 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SALAH APIGA MBILI LIVERPOOL YAICHAPA BRIGHTON 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top