• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 23, 2020

  DOMAYO AFUNGA BAO PEKEE AZAM FC YAICHAPA MBEYA CITY 1-0 NA KUREJEA NAFASI YA PILI LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la kiungo Frank Raymond Domayo dakika ya 70 limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 69 na kurejea nafasi ya pili, sasa ikiwazidi wastani wa mabao tu, vigogo Yanga SC baada ya timu zote kucheza mechi 37.  
  Sasa mshindi wa pili wa Ligi Kuu atajulikana baada ya mechi za mwisho zitakazochezwa mwishoni mwa wiki, kwani tayari bingwa amekwishapatikana, Simba SC aliyetwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo mapema Juni 28 akiwa amebakiza mechi sita.


  Baada ya sare ya 0-0 na Coastal Unon leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Simba SC, mabingwa mara 21 wa Ligi Kuu wamefikisha pointi 85, sasa wakiwazidi pointi 16 Azam na watani wao wa jadi, Yanga SC kuelekea mechi za mwisho.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Abdul Omary/Joseph Mahundi dk9, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Abdallah Kheri, Mudathir Yahya/Brayson Raphael dk89, Iddi Suleiman ‘Nado’, Frank Domayo, Obrey Chirwa, Rchard Ella D’jodi/Andrew Simchimba dk68 na Never Tegere/Oscar Maasai dk90+5.
  Mbeya City; Haroun Mandanda, Kenneth Kunambi, Mpoki Mwaknyuke, Feisal Mganga, Rolland Msonjo, Samson Madeleke, Edger Mbembela, Abdul Suleiman, Abasarim Chidiebere, Peter Mapunda/Patson Shigala dk7 na Daniel Lukandamila/Gamba Iddy dk90+4.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DOMAYO AFUNGA BAO PEKEE AZAM FC YAICHAPA MBEYA CITY 1-0 NA KUREJEA NAFASI YA PILI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top