• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 29, 2020

  IHEFU YABISHA HODI LIGI KUU BAADA YA KUIPIGA MBAO FC 2-0, MBEYA CITY YAJIWEKA NJIA PANDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Ihefu FC imebisha hodi Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mabo FC ya Mwanza katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania Uwanja wa Highland Estae, Mbalizi mkoani Mbeya.
  Mabao ya Ihefu yamefungwa na Steven Mwaijala kwa penalti dakika ya nne na Mridi Tangai dakika ya 4 na sasa watahitaji kuulinda ushindi wao kwenye mchezo wa marudiano Jumapili Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza ili kupanda Ligi Kuu.
  Mbeya Cty walitangulia kwa bao la Suleiman Ibrahim dakika ya 41, kabla ya wenyeji, Geita Gold kusawazisha dakika ya 68 kwa bao la kujifunga la Rehani Kibingu.
  Nayo Mbeya Cty imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Geita Gold Uwanja wa sekondari ya Nyankungu katika mchezo mwingine wa mchezo (Play-Offs) leo.
  Mbeya City watahitaji kushinda nyumbani Jumapili Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya kwenye mchezo wa marudiano ili kubaki Ligi Kuu.
  Mbeya City na Mbao FC zilimaliza nafasi ya 15 na 16 katika Ligi Kuu, hivyo kulazimika kucheza na timu zilizoshika nafasi ya pili kwenye makundi A na B Daraja la Kwanza kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: IHEFU YABISHA HODI LIGI KUU BAADA YA KUIPIGA MBAO FC 2-0, MBEYA CITY YAJIWEKA NJIA PANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top