• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 06, 2020

  MANDZUKIC AVUNJA MKATABA NA AL-DUHAIL BAADA YA MIEZI SITA TU

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Juventus, Mario Mandzukic amevunja mkataba na klabu ya Al-Duhail baada ya miezi sita tu tangu ajiunge nayo. 
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alihamia Qatar Desemba mwaka jana baada ya kupoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Maurizio Sarri, Juve.
  Lakini Mcroatia huyo aliyefunga bao la ushindi dhidi ya England kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2018, sasa yuko huru baada ya kuthibitisha kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba amevunja mkataba na klabu hiyo ya Mashariki ya Kati kwa maridhiano. 

  Mario Mandzukic amevunja mkataba na Al-Duhail ya Qatar baada ya miezi sta tu 

  Mandzukic amecheza mechi tano Al-Duhail katika Ligi ya Qatar, lakini ameshindwa kufunga hata bao moja katika kipindi chake kifupi cha kuwa na timu hiyo katika mashindano ya nchini humo.  
  Alifanikiwa kufunga bao moja kwenye Ligi ya Mabingwa ya Asia dhidi ya Persepolis Februari 11.  
  Kabla ya kuhamia Mashariki ya Kati, kocha wa Juventus, Sarri hakumtumia Mandzukic kwenye kikosi cha kwanza na alikuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa na kujiunga na Manchester United.
  Alikuwa ana wakati mzuri chin ya kocha aliyetangulia Juve, Massimiliano Allegri na akaisaidia timu hiyo kushinda mataji manne ya Serie A na matatu ya Coppa Italia alipokuwa na klabu hiyo. 
  Mandzukic pia alifunga tik-tak ya kukumbukwa kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa 2017 dhidi Real Madrid, ambayo hata hvyo iliibuka na ushindi wa 4-1. 
  Sasa anahusishwa na kurejea Italia huku AC Milan na vinara wa Serie B, Benevento wote wakitajwa kumuwania mchezaji huyo pamoja na Galatasaray na Fenerbahce za Uturuki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANDZUKIC AVUNJA MKATABA NA AL-DUHAIL BAADA YA MIEZI SITA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top