• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 04, 2020

  NAMUNGO FC YAICHAPA 1-0 JKT TANZANIA RUANGWA NA KUFIKISHA POINTI ZA AZAM LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, RUANGWA
  TIMU ya Namungo FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Kwa ushindi huo ulitokana na bao pekee la Abeid Athumani dakika ya 34, Namungo FC inafikisha pointi 59 baada ya kucheza mechi 33, sasa ikilingana na Azam FC yenye mechi moja mkononi, ambayo hata hivyo inabaki nafasi ya tatu kwa wastani mzuri wa mabao. 
  Tayari Simba SC ni mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo kutokana na pointi zao 79, wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 60 baada ya wote kucheza mechi 32.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, KMC imeichapa 3-2 Mwadui FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam na Kagera Sugar imelazimishwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  Nayo Mbao FC imechapa 2-0 Lipuli FC Uwanja wa CCM Kirumba Jijin Mwanza na Tanzania Prisons imelazimishwa sare ya 0-0 na Polisi Tanzania Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAICHAPA 1-0 JKT TANZANIA RUANGWA NA KUFIKISHA POINTI ZA AZAM LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top