• HABARI MPYA

  Tuesday, July 21, 2020

  RONALDO APIGA MBILI JUVENTUS YAICHAPA LAZIO 2-1 SERIE A

  Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Juventus, kwa penalti dakika ya 51 na lingine dakika ya 54 akimalizia pasi ya Paul Dybala katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Lazio ambayo bao lake lilifungwa na Ciro Immobile dakika ya 83. Ushindi huo unaifanya Juventus ifikishe pointi 80 na kuendelea kuongoza Serie A kwa pointi nane zaidi ya Inter Milan inayofuatia baada ya wote kucheza mechi 34, wakat Lazio inabaki nafasi ya nne na pointi zake 69 za mechi 34 pia. Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 50 kwenye Serie A, Lg Kuu England na La Liga PICHA ZAIDI GONGA HAPA    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO APIGA MBILI JUVENTUS YAICHAPA LAZIO 2-1 SERIE A Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top