• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 26, 2020

  SAMATTA AINUSURU ASTON VILLA KUSHUKA DARAJA BAADA YA SARE YA 1-1 NA WEST HAM UNITED

  Na Mwandishi Wetu, LONDON
  MSHAMBULIAJI wa kimatiafa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amekuwa sehemu ya kikosi cha Aston Villa kilichoinusuru timu hiyo kushuka daraja baada ya sare ya 1-1 na wenyeji, West Ham United Uwanja wa London.
  Samatta alicheza kwa dakika 68 mchezo huo wa Ligi Kuu ya England kabla ya kumpisha chipukizi wa England, Keinan Davis wakati huo timu hizo hazijafungana.
  Nyota wa England, Jack Grealish alianza kuifungia Aston Villa dakika ya 84 akimalizia pasi ya kiungo mwenzake, Mscotland John McGinn bao lililodhaniwa litakuwa la ushindi.
  Mbwana Samatta amekuwa sehemu ya kikosi cha Aston Villa kilichoinusuru timu yao kushuka daraja leo 

  Lakini mshambuliaji wa kimataifa wa Ukraine Andriy Yarmolenko akaisawazishia West Ham United dakika ya 85 akimalizia pasi ya kiungo wa England, Declan Rice.  
  Kwa matokeo hayo, Aston Villa inakamilisha msimu wa Ligi Kuu ya England na pointi 35, ikizizidi pointi moja moja AFC Bournemouth na Watford zilizoungana na Norwich City kushuka daraja.  
  Pamoja na kufanya vibaya katika Lg Kuu, lakini Villa walikuwa na msimu mzuri kwenye Kombe la Ligi ambako walifika fainali na kufungwa 2-1 na Manchester City Machi 1 Uwanja wa Wembley, Samatta akifunga bao la kufutia machozi dakika ya 41 baada ya Sergio Aguero na Rodri kutangula kufunga dakika ya 20 na 30.
  Kikosi cha West Ham United kilikuwa; Fabianski, Fredericks, Ogbonna, Diop, Johnson, Rice, Soucek, Fornals/Lanzini dk67, Noble/Anderson dk87, Bowen/Yarmolenko dk46 na Antonio/Haller dk46.
  Aston Villa; Reina, Targett, Konsa, Mings, Guilbert/Hause dk76, Hourihane/Nakamba dk72, Luiz, McGinn, Grealish, Samatta/Davis dk68 na Trezeguet/El Ghazi dk90.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AINUSURU ASTON VILLA KUSHUKA DARAJA BAADA YA SARE YA 1-1 NA WEST HAM UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top