• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 10, 2020

  SAMATTA AANZISHWA, ATOLEWA ASTON VILLA YAMIMINIWA 3-0 NA MANCHESTER UNITED VILLA PARK

  Na Mwandishi Wetu, BIRMINGHAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana ameanzishwa timu yake, Aston Villa ikichapwa 3-0 na Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Villa Park.
  Samatta alicheza kwa dakika 59 tu jana kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na chikupizi wa England, Keinan Davis.
  Na Samatta alitolewa wakati tayari Aston Villa imekwisharuhusu mabao hayo matatu, yaliyofungwa na Bruno Fernandes dakika ya 27 kwa penalti baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Ezri Konsa, Mason Greenwood dakika ya 45 na Paul Pogba dakika ya 58.
  Kwa ushindi huo Manchester United inafikisha pointi 58, ingawa inabaki nafasi ya tano, ikizidiwa pointi moja na Leicester City baada ya wote kucheza mechi 34. 
  Aston Villa inayobaki na pointi zake 27, baada ya kuruhusu mabao matatu jana inateremka kwa nafasi moja tena hadi ya 19, ikiizidi pointi sita Norwich City inayoshika mkia.
  Kikosi cha Aston Villa kilikuwa: Reina; Konsa, Hause, Mings, Taylor; El Ghazi/Hourihane dk59, Luiz/Vassilev dk84, McGinn/Nakamba dk59, Trezeguet, Grealish na Samatta/Davis dk59.
  Manchester United: De Gea, Wan-Bissaka/Williams dk66, Lindelof, Maguire, Shaw, Pogba, Matic/McTominay dk66, Greenwood/James dk80, Fernandes/Fred dk71, Rashford na Martial/Ighalo dk79.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AANZISHWA, ATOLEWA ASTON VILLA YAMIMINIWA 3-0 NA MANCHESTER UNITED VILLA PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top