• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 17, 2020

  SAMATTA AANZA, ATOLEWA ASTON VILLA YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA WENYEJI, EVERTON GOODISON PARK

  Na Mwandishi Wetu, LIVERPOOL
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amecheza kwa dakika 63, Aston Villa ikilazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Everton Uwanja wa Goodison Park Jijini Liverpool.
  Samatta, mchezaji wa zamani wa African Lyon na Simba za Tanzania, alitoka dakika ya 63 kumpisha  KeinanDavis, wakati huo timu hizo bado hazijafungana.
  Na akiwa benchi, Samatta akashuhudia Aston Villa ikitangulia kwa bao la Ezri Konsa dakka ya 72 akimalizia pasi ya Conor Hourihane kabla ya Theo Walcott kuisawazishia Everton dakika ya 87 akimalizia pasi ya Andre Gomes.
  Sasa Aston Villa inafikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi 36, ingawa inabaki nafasi ya 19, ikizidiwa wastani wa mabao tu na AFC Bournemouth inayoshika nafasi ya 18.
  Kikosi cha Everton kilikuwa: Pickford, Coleman, Keane, Holgate/Branthwaite dk15, Digne, Iwobi/Walcott dk61, Gomes, Davies, Bernard/Gordon dk61, Richarlison/Kean dk73, Calvert-Lewin.
  Aston Villa: Reina, El Mohamady, Konsa, Mings, Targett, McGinn, Luiz, Hourihane, Trezeguet/El Ghazi dk63, Grealish, Samatta/Davis dk63.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AANZA, ATOLEWA ASTON VILLA YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA WENYEJI, EVERTON GOODISON PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top