• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 12, 2020

  STERLING APIGA HAT TRICK MAN CITY YAICHAPA BRIGHTON 5-0

  Raheem Sterling (kushoto) akipongezwa na mwenzake baada ya kuifungia Manchester City mabao matatu dakika za 21,53 na 81 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa AMEX. Mabao mengine ya Manchester City yalifungwa na Gabriel Jesus dakika ya 44 na Bernardo Silva dakika ya 56 na kwa ushindi huo, kikosi cha Pep Guardiola kinafikisha pointi 72 na kuendelea kukamata nafasi ya pili, nyuma ya mabingwa tayari, Liverpool wenye pointi 93 baada ya wote kucheza mechi 35 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STERLING APIGA HAT TRICK MAN CITY YAICHAPA BRIGHTON 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top