• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 04, 2020

  GREENWOOD APIGA MBILI MAN UNITED YAICHAPA BOURNEMOUTH 5-2

  Mason Greenwood akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Manchester United katika ushindi wa 5-2 dhidi ya AFC Bournemouth leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford. Mabao mengine ya Man United yamefungwa na Marcus Rashford kwa penalti dakika ya 35, Anthony Martial dakika ya 45 na ushei na Bruno Fernandes dakika ya 59, wakati ya Bournemouth yamefungwa na Junior Stanislas dakika ya 15 na Joshua King dakika ya 49 kwa penalti. Kwa ushindi huo, Man United inafikisha pointi 55 baada ya kucheza mechi 33 na kupanda nafasi ya nne, sasa ikiizidi pointi moja Chelsea ambayo baadaye inacheza mechi yake ya 33 dhidi ya Watford 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GREENWOOD APIGA MBILI MAN UNITED YAICHAPA BOURNEMOUTH 5-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top