• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 22, 2020

  SAMATTA APAMBANA ASTON VILLA YAICHAPA ARSENAL 1-0 NA KUJIONDOA ENEO LA HATARI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana alicheza kwa dakika 72 timu yake, Aston Villa iikibuka na ushindi 1-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Vlla Park.
  Ni ushindi waliouhitaji Aston Villa katika harakati zao za kujinusuru kushuka daraja na sasa wanafikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 37 na wanapanda kwa nafasi moja hadi ya 17, sasa wakiizidi wastani wa mabao tu Watford.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa, Chris Kavanagh wa Lancashire, bao pekee la Aston Villa lilifungwa na kiungo Mmisri, Mahmoud Ahmed Ibrahim Hassan, maarufu kama Trezeguet dakika ya 27 akimalizia kazi nzuri ya Tyrone Mings.
  Mbwana Samatta (kulia) akipambana na walinzi wa Arsenal usiku wa jana Uwanja wa Villa Park 

  Kocha Dean Smith alimpumzisha Samatta dakika ya 72 nafasi yake ikichukuliwa na kinda wa England, Keinan Davis aliyekwenda kumalizia kazi vizuri timu ikiulinda ushindi wake na kuvuna pointi tatu muhimu.
  Aston Villa watakamilisha mechi zao za msimu Jumapili kwa mchezo wa ugenini dhidi ya West Ham United Uwanja wa London kuanzia Saa 12:00.
  Kikosi cha Aston Villa kilikuwa: Reina, Elmohamady/Guilbert dk25, Konsa, Mings, Targett, McGinn/Lansbury dk90, Douglas Luiz, Hourihane/Nakamba dk73, Trezeguet, Samatta/Davis dk72 na Grealish.
  Arsenal: Martinez, Holding, Luiz/Pepe dk60, Kolasinac, Cedric/Willock dk79, Ceballos, Torreira/Xhaka dk46, Saka/Tierney dk60, Nketiah, Lacazette na Aubameyang.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA APAMBANA ASTON VILLA YAICHAPA ARSENAL 1-0 NA KUJIONDOA ENEO LA HATARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top