• HABARI MPYA

  Tuesday, July 21, 2020

  DIAMOND PLATNUMZ NA PARIMATCH WAVIPGA JEKI VITUO VIWILI VYA MAKAO DAR ES SALAAM

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya Parimatch imevipiga jeki vituo viwili vya makao ambavyo ni Huruma Islamic pamoja na Amani Foundation vilivyopo katika jiji la Dar es Salaam. 
  Katika mahitaji yao wamewapa chakula na nyenzo za kujifunza ili kuweza kuendana na kasi ya teknolojia na kujiandaa vyema na mahitaji ya soko la ajira au kujiajiri kwa kuwapa runinga, jenereta pamoja na Mifumo kamilifu itakayounda maabara za Kompyuta ili kusudi viweze kuwaendeleza katika masuala ya elimu na kujifunza.
  Akizunguma na Waandishi wa Habari leo katika hafla iliyohudhuriwa na Balozi wao, mwanamuziki Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ – Mkurugenzi Mtendaji wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana amesema kwamba wanapenda umma utambue kuwa kampuni yao imejengwa katika misingi ya kusaidia jamii hususani katika nyanja za elimu, michezo, na mazingira. 


  “Brand ya Parimatch inaendesha shughuli michezo ya kubashiri kitaifa na kimataifa ambapo kwa sasa ipo takribani mataifa 15 ikiwa na wachezaji zaidi ya milioni moja. Na nguzo yetu kuu ni kujali na kukilinda kizazi cha baadae. Hivyo basi kwa leo tunaanza na idara ya elimu kwa watoto wenye mahitaji muhimu kwa kuangazia baadhi ya mahitaji yao,”. 
  “Jambo la Pili, katika sekta ya michezo tunazindua rasmi kampeni yetu ya AMSHA NDOTO NA PARIMATCH ambayo kila mwezi kutakuwa na droo Maalum itakayowezesha timu shiriki kujipatia vifaa vya michezo kutoka Parimatch,”.
  “Ili timu hizi ziweze kupata nafasi zitatakiwa kutembelea tovuti yetu ya https://pma.bet/amshandoto kujaza fomu ya ushiriki na viambatanisho husika na kila mwezi tutachagua timu hadi 5 za zitakazopatiwa vifaa ikiwemo jezi, viatu, mipira na bibs. Kwa timu tano kwa mwezi hivyo kwa mwaka tunaweza fikia karibu timu 60 jambo ambalo sio dogo katika kukuza sekta hii ya michezo,”.
  “Mbali na hayo, pia jamii inapaswa itambue kuwa ni jukumu la kila mtu kuhakikisha anasaidia jamii inayoishi katika mazingira ya makao ili kusudi kuweka usawa  katika jamii na maisha kiujumla.
  Diamond Press,”

  “Mada kuu za Diamond kuongelea:
  1. Parimatch iko katika misingi ya kusaidia jamii katika nchi zote ambayo ipo na ipo zaidi ya nchi 15.Misingi hii iko katika nyanja za elimu, michezo na mazingira.
  2. Hivyo leo tupo na viongozi wa makao (vituo vya watoto wenye mahitaji muhimu) kama ishara ya program endelevu kusaidia jamii, vituo vya makao kwa dar es salaam vipo zaidi ya 40. Tutaanza na vituo viwili kuwapa mahitaji ya chakula ambayo bila hivyo huwezi kusoma, lakini mada kuu elimu. Katika elimu sasa tunawatengenezea maabara ya kompyuta yenye kompyuta 10 au zaidi kwa kila kituo na luninga mbili mbili ili hawa nao wasome kitandawazi, wasome kwa fursa sawa kama watoto wengine sio unafundishwa kompyuta kwa kuchorewa ubaoni. Na mkikwama milango iko wazi karibuni
  3. Pili na kubwa, ni katika nyanja ya michezo. Leo tunaanzisha rasmi program inaitwa AMSHA NDOTO. Kuna tovuti yetu www.amshandoto.parimatch.co.tz ambapo vijana wenye timu yenu iko mtaani na mna mahitaji ya jezi, vifaa vya mazoezi mnaeza tembelea mkajaza taarifa zenu. Kila mwezi Parimatch itatoa vifaa kwa timu hadi 5 hivyo kwa mwaka ni kama timu 60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIAMOND PLATNUMZ NA PARIMATCH WAVIPGA JEKI VITUO VIWILI VYA MAKAO DAR ES SALAAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top