• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 05, 2020

  SAMATTA ATOKEA BENCHI BADO DAKIKA 16 ASTON VILLA YACHAPWA 2-0 NA LIVERPOOL ANFIELD

  Na Mwandishi Wetu, LIVERPOOL
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ametokea benchi bado dakika 16 leo timu yake, Aston Villa ikichapwa 2-0 na Liverpool Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Samatta aliingia uwanjani dakika ya 74 kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa England, Keinan Davis wakati huo tayari Liverpool inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Msenegal, Sadio Mane dakika ya 71.
  Na akiwa uwanjani, Samatta aliyejunga na Aston Villa Januari akitokea KRC Genk ya Ubelgiji, timu yake ya kwanza Ulaya aliyojiunga nayo mwaka 2016 akashuhudia Liverpool wakipata bao la pili lililofungwa na kinda Curtis Jones dakika ya 89.
  Liverpool ambao tayari ni mabingwa, kwa ushindi wa leo wanafikisha pointi 89 baada ya kucheza mechi 33, wakati Aston Villa ya kocha Dean Smith inabaki na nafasi ya 19 na pointi zake 27 baada ya kucheza mechi 33 pia – maana yake inaanza kuipungia mkono wa kwaheri Ligi Kuu.
  Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Alisson, Alexander-Arnold, Gomez, Van Dijk, Robertson, Oxlade-Chamberlain/Wijnaldum dk60, Fabinho/Henderson dk60, Keita, Salah, Origi/Firmino dk60 na Mane.
  Aston Villa; Reina, Konsa, Hause, Mings, Taylor, El Ghazi/Jota dk74, McGinn, Luiz, Trezeguet/Vassilev dk84, Grealish na Davis/Samatta dk74.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI BADO DAKIKA 16 ASTON VILLA YACHAPWA 2-0 NA LIVERPOOL ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top