• HABARI MPYA

  Wednesday, July 15, 2020

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA AZAM FC 1-0 GAIRO NA KUFUFUA MATUMANI YA KUBAKI LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, GAIRO
  TIMU ya Mtibwa Sugar imeutumia vyema Uwanja wa nyumbani, CCM Gairo mkoani Morogoro baada ya ushindi wa 1-0 dhidi Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ dakika ya 38 na kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 35 na kupanda hadi nafasi ya 13 kutoka ya 17.
  Azam FC wao wanabaki nafasi ya pili na pointi zao 65 za mechi 35 sasa, ingawa wanaweza kuangukia nafasi ya tatu iwapo Yanga SC wataifunga Singida United baadaye leo.


  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Namungo FC imeichapa Mbeya City 1-0, bao pekee la Abeid Athumani dakika ya 46 Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Pwani.
  Na Uwanja wa Kaitaba, Bukoba bao la penalti la Awesu Awesu dakika ya 40 limeipa ushindi wa 1-0 Kagera Sugar dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
  Bao la Adam Adam dakika ya 90 na ushei likaipa sare ya 1-1 nyumbani JKT Tanzania dhidi ya Alliance FC ya Mwanza iliyotangulia kwa bao la David Richard dakika ya 36 Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Nayo Ndanda FC ikaichapa 2-1 Tanzania Prisons Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Mabao ya Ndanda yalifungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 39 na Taro Donald dakika ya 51, wakati la Prisons limefungwa na Jumanne Elifadhili kwa penalti dakika ya 65.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA AZAM FC 1-0 GAIRO NA KUFUFUA MATUMANI YA KUBAKI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top