• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 06, 2020

  MIKE TYSON ANAAMINI WILDER ANAWEZA KULIPA KISASI KWA FURY

  GWIJI wa ndondi, Mike Tyson anaamini Mmarekani mwenzake, Deontay Wilder ana nafasi ya kushinda dhidi ya Tyson Fury iwapo watarudiana tena.
  Pambano la kwanza la Wilder na Fury lilimalizika kwa droo kabla ya wawili hao kupigana tena Las Vegas Februari ambako Muingereza akashinda na kutwaa taji la WBC uzito wa juu.  
  Pambano lao la tatu linatarajiwa kufanyika Desemba na alipoulizwa na rapa Fat Joe kwenye Instagram kama Wilder anaweza kushinda pambano lijalo, Tyson alisema: "Wakati wowote kuna nafasi. Kila mmoja wakati wote ana nafas. Itategemea na kiasi gani atajitoa,".

  Mike Tyson anaamini Deontay Wilder ana nafasi ya kulipa kisasi kwa Tyson Fury wakirudiana tena PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  "Ikiwa atataka kuyatoa maisha yake kwa ajili ya kushinda haswa pambano hili, chochote kinaweza kutokea,".
  Pambano la tatu la Fury na Wilder linaweza kufanyika Uwanja mpya wa Allegiant Jijini Las Vegas, ingawa taarifa za mwisho hazijatolewa japo imependekezwa lifanyike Desemba 19.
  Uwanja huo wa NFL uliogharmu dola za Kimarekani Bilioni 1.45 ujenzi wake, unaingiza watazamaji 65,000 lakini wataruhusiwa kuingia watu 20,000 tu kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya corona.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MIKE TYSON ANAAMINI WILDER ANAWEZA KULIPA KISASI KWA FURY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top