• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 11, 2020

  MBEYA CITY YAICHAPA POLISI TANZANIA 2-1 SOKOINE, LAKINI BADO IPO HATARINI KUSHUKA DARAJA

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  TIMU ya Mbeya City jana imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Mbeya City katika mchezo wa jana yalifungwa na Rolland Msonjo dakika ya 36 na Peter Mapunda dakika ya 89, wakati la Polisi Tanzania lilifungwa na  Shaaban Stambuli dakika ya 26
  Kwa ushindi huo, Mbeya City inayofundishwa na kocha Amri Said ‘Stam’ inafikisha pointi 39 baada ya kucheza mechi 34.
  Polisi Tanzania yenyewe inabaki na pointi zake 48 za mechi 34 katika nafasi ya sita, ikizidiwa pointi tatu na Coastal Union ya Tanga inayoshika nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAICHAPA POLISI TANZANIA 2-1 SOKOINE, LAKINI BADO IPO HATARINI KUSHUKA DARAJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top