• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 17, 2020

  JAMAL KHALFAN ABDALLAH AKABIDHIWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 288 BAADA YA KUSHINDA JACKPOT SPORTPESA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya Michezo na Burudani ya SportPesa Tanzania leo imemkabidhi mshindi wa Jackpot SportPesa, Jamal Khalfan Abdallah Shilingi 288, 974, 720 baada ya kuibuka mshindi.
  Hii ni awamu ya nne kwa Jackpot ya SportPesa kupata mshindi kutoka wilaya ya Ilala, Dar baada ya washindi wengine watatu kujizolea mamilioni kupitia ubashiri huo wa michezo. 
  Jamal mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa Ilala jijini Dar-es-Salaam, amejishindia kiasi hicho cha pesa baada ya kubashiri mechi 13 za Jackpot kwa usahihi.
  Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas akimkabidhi Jamal Khalfan Abdallah mfano wa hundi ya Sh 288, 974, 720 baada ya kushinda.
  Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas akiwa na Jamal Khalfan Abdallah na wachezaji wa Yanga

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kumtangaza mshindi huyo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Bwana Tarimba Abbas alisema kuwa Bw. Jamal ameshinda Jackpot hiyo baada ya kubashiri mechi 13 zilizochezwa mwishoni mwa wiki kwa usahihi.
  “Mpaka sasa SportPesa imeshatoa zaidi ya Sh Bil 1.8 kwa washindi wanne wa jackpot kwa kubashiri kwa usahihi mechi 13. Pia tangu tuanze biashara Mei, 2017 hadi leo hii washindi wa Jackpot na bonasi wamelipwa zaidi ya Bil 8.2.
  “Tunafurahi kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kubajdili Maisha ya Watanzania mbalimbali na kuongeza familia ya mamilionea,” alisema Tarimba na kuongeza kuwa.
  “SportPesa ni kampuni inayofuata taratibu zote ili kuhakikisha sheria zilizowekwa na bodi ya michezo ya kubahatisha zinafutwa ikiwa pamoja na kulipa kodi. Kodi iliyolipwa kwa washindi wote wa Jackpot waliopatikana kuanzia 2017 tu eweza kurudisha kodi kwa serikali kwa zaidi ya shilingi Bilioni 1.6.
  “Nitoe rai kwa Watanzania wote na wapenda michezo kuwa SportPesa ipo kwa ajili ya kuwaburidisha hasa kwenye ubashiri wa mipira ya miguu na mara zote mshindi uwekewa pesa zake kwenye akaunti yake papo hapo,” alisema Tarimba.
  Akizungumza mara baada ya ushindi wake, Jamal alisema kuwa “Sikutegemea kama nitashinda maana niliwekea mikeka zaidi ya kumi, hivyo nilitegemea kupata bonasi na sio Jackpot.
  “Hizi pesa nilizoziweka kwa hivi sasa sitazitumia na badala yake nitaziweka kwanza benki kwa muda huku nikifikiria nini cha kufanya, kwa sababu hizi pesa ni nyingi kwani utulivu mkubwa unahitajika.
  “Mimi ninajishughulisha na ujasiliamali kwa hivi sasa, hivyo kupitia ushindi wangu huu ninaamini nitafanikisha mahitaji yangu muhimu,”
  “Pesa nilizoshinda nimelipa shilingi 57,794,944/- kama kodi kwa serikali na kiasi kilichobakia ambacho ni zaidi ya Mil 231 nitapunguza pia asilimia 10 na kutoa msaada kwa watoto yatima.
  “Nashabikia sana timu ya Young Africans na nimefurahi sana SportPesa kuniletea wachezaji kama suprise ya leo.”
  Wawakilishi kutoka Bodi ya michezo ya kubashiri Humoud Abdul na Masoud Yasur walihudhuria kwa umakini mkutano huo ili kuhakikisha taratibu na kanuni za bodi hiyo zinafuatwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JAMAL KHALFAN ABDALLAH AKABIDHIWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 288 BAADA YA KUSHINDA JACKPOT SPORTPESA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top