• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 18, 2020

  DODOMA FC WAICHAPA 1-0 GWAMBINA NA KUTWAA UBINGWA LIGI DARAJA LA KWANZA TZ BARA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Dodoma FC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara baada ya ushindi 1-0 dhidi ya Gwambina FC, bao pekee la Anuary Jabir dakika ya 52 leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Fainali hiyo tamu ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilihusisha washindi wa makundi mawili katika hatua ya awali Dodoma FC kutoka Kund B dhidi ya Gwambina FC ya Misungwi mkoani Mwanza kutoka Kund B.
  Kwa kuongoza tu makundi yao, kwa pamoja timu hizo zilijihakikishia tiketi ya kucheza Ligi Kuu – huku  Ihefu FC ya Mbarali mkoani Mbeya na Maji Maji ya Songea mkoani Ruvuma kutoka kundi A na Geita Gold ya Geita na Trans Camp ya Dar es Salaam kutoka kundi B zikifuzu kucheza mechi za mchujo (Play Off) ya kuwania kupanda Ligi Kuu. 


  Mlale FC, Pan African, Cosmopolitan FC na Iringa United zimeshuka daraja la pili (SDL) kutoka kundi A huku Timu za Boma FC na Friend Rangers zitacheza play off ya kubaki ligi Daraja la kwanza au kushuka Daraja la Pili (SDL) kutoka kundi A
  Green Warriors, Sahare All Stars, Stand United na Mawenzi Market FC zote zimeshuka daraja kwenda daraja la Pili  (SDL) kutoka kundi B huku Mashujaa na  Pamba/Arusha FC zitacheza play off ya kubaki daraja la kwanza au kushuka Daraja la Pili kutoka kundi B.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DODOMA FC WAICHAPA 1-0 GWAMBINA NA KUTWAA UBINGWA LIGI DARAJA LA KWANZA TZ BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top