• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 31, 2020

  AKINA MSUVA WALAZIMISHWA SARE YA PILI MFULULIZO YA BILA KUFUNGANA LIGI KUU YA MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, MAZGHAN
  KUINGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana kwa mara nyingine alishindwa kuisaidia timu yake, Difaa Hassan El-Jadidi kuondoka na pointi zote tatu baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na Ben Ahmed El Abdi, El Jadida mjini Mazghan, Casabablanca. 
  Sare hiyo inafuatia sare nyingine ya 0-0 na Raja Casabablanca hapo hapo Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Morocco baada ya kurejea kufuatia kusimama tangu Machi kutokana na  mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona.
  Na Msuva (pichani kulia), mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam alicheza mechi zote hizo mbili kwa ustadi mkubwa kama kawaida yake – lakini tu bahati haikuwa yake kuweza kufunga.
  Na baada ya sare hizo mbili mfululizo, Difaa Hassan El-Jadidi inafikisha pointi 27 kufuatia kucheza mechi 20 za Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro na kupanda kwa nafasi moja hadi ya nane, sasa ikiizidi pointi tatu Youssoufia Berrechid.
  Difaa Hassan El-Jadidi watateremka tena uwanjani Agosti 11 katika mchezo wa tatu mfululizo wa nyumbani wa Ligi ya Morocco wakimenyana na FAR Rabat Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi, El Jadida mjini Mazghan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AKINA MSUVA WALAZIMISHWA SARE YA PILI MFULULIZO YA BILA KUFUNGANA LIGI KUU YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top