• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 05, 2020

  AZAM FC YAREJEA NAFASI YA PILI LIGI KUU BAADA YA KUITANDIKA SINGIDA UNITED 7-0 CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imerejea nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 7-0 dhidi ya Singida United usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Azam FC inayofundishwa na kocha Aristica Cioaba kutoka Romania inafikisha pointi 62 baada ya ushindi huo, sasa ikiwazidi pointi moja, vigogo Yanga SC wanaofuatia nafasi ya tatu baada ya timu zote kucheza mechi 33.  
  Mabingwa tayari kwa mara ya tatu mfululizo, Simba SC wapo kileleni kwa pointi zao 80 baada ya kucheza mechi 33 pia.


  Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na kiungo, Iddi Suleiman ‘Nado’ mawili, David Natley aliyejifunga dakika ya 41 na mshambuliaji wake Mzambia, Obrey Chirwa aliyefunga manne dakika za 44, 55, 56 na 62.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, mabingwa Simba SC wamelazimishwa sare ya 0-0 pia na Ndanda SC Uwanja wa Nangwanda SIjaona Mtwara na vigogo, Yanga SC wamelazimishwa sare ya bila kufungana pia na wenyeji, Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
  Nayo Alliance FC imelazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar ya Morogoro Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza, wenyeji wakitangulia kwa bao la kujifunga la Henry Joseph dakika ya kwanza kabla ya Salum Kihimbwa kuwasawazishia wagen dakika ya 55.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAREJEA NAFASI YA PILI LIGI KUU BAADA YA KUITANDIKA SINGIDA UNITED 7-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top