• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 08, 2020

  VARDY AISAWAZISISHIA LEICESTER BADO DAKIKA SITA, SARE 1-1 NA ARSENAL

  Jamie Vardy akishangilia baada ya kuifungia bao la kusawazsisha Leicester City dakika ya 84 ikitoa sare ya 1-1 na Arsenal iliyotangulia kwa bao la Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 21 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Emirates. Arsenal ilimaliza pungufu baada ya Eddie Nketiah kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 74, dakika nne tu tangu aingie kuchukua nafasi ya Alexandre Lacazette. Leicester inafikisha pointi 59 baada ya sare hiyo katika mchezo wa 34 na sasa inashuka hadi nafasi ya nne ikizidiwa pointi moja na Chelsea, wakati Arsenal inayofikisha pointi 50 baada ya kucheza mechi 34 pia inabaki nafasi ya saba 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VARDY AISAWAZISISHIA LEICESTER BADO DAKIKA SITA, SARE 1-1 NA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top