• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 22, 2020

  STERLING APIGA MBILI MAN CITY YAICHAPA WATFORD 4-0

  Raheem Sterling usiku wa jana amefunga mabao mawili dakika za 31 na 40 Manchester City ikiichapa Watford 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England, mabao mengine yakifungwa na Phil Foden dakika ya 63 na Aymeric Laporte dakika ya 66 Uwanja wa Vicarage Road. Man City inafikisha pointi 78 baada ya ushindi huo kwenye mchezo wa 37, ingawa inabaki nafasi ya pilo nyuma ya mabingwa tayari, Liverpool wenye pointi 93 za mechi 36, wakati Watford inayobaki na pointi zake 34 baada ya mechi 37 pia, inashuka kwa nafasi moja hadi ya 18 sasa ikiwa hatarini zaidi kushuka daraja 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STERLING APIGA MBILI MAN CITY YAICHAPA WATFORD 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top