• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 28, 2020

  CLATOUS CHAMA NA FEISAL SALUM WA YANGA SC WASHINDA TUZO YA MACHEZAJI BORA WA MSIMU SPORTPESA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  VIUNGO, Mzambia Clatous Chama wa Simba SC na Feisal Salum wa Yanga SC wameshinda tuzo za Machezaji Bora wa Msimu wa klabu zao baada ya zoezi la upigaji kura kwa mashabiki lililoendeshwa na kampuni hiyo.
  Taarifa ya SportsPesa kupitia ukurasa wake wa Instagram leo imesema;  “Hongereni sana Clatous Chama kuwa SportPesa Mchezaji Bora wa Msimu kutoka Simba na Fei Toto kuwa SportPesa Mchezaji Bora wa msimu kutoka Yanga. Kura nyingi ndio ziliamua ushindi huu kwa pande zote mbili. 
  Lakini taarifa hiyo haikusema wawili hao watapewa zawadi gani kwa ushindi wao huo zaidi ya kumaliza kwa kusema; “Hii ni Zawadi toka kwa Mdhamini Mkuu wa Vilabu vyote viwili,”.
  Wakati Chama ameisaidia Simba SC kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mzanzibari Feisal Salum ameiwezesha Yanga SC kumaliza katika nafasi ya pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CLATOUS CHAMA NA FEISAL SALUM WA YANGA SC WASHINDA TUZO YA MACHEZAJI BORA WA MSIMU SPORTPESA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top