• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 13, 2020

  HAIKUFUNGWA YANGA, BALI KOCHA NA BENCHI LAKE ZIMA LA UFUNDI

  Na Makusudi Lubosangija, MWANZA
  VIGOGO, Yanga SC jana walitupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuchapwa 4-1 na watani wao, Simba SC Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
  Simba SC sasa inakwenda fainali na itakutana na Namungo FC iliyoitoa Sahare All Stars kwa kuichapa 1-0, mchezo ambao utapigwa Agosti 2 Uwanja wa Mandela, Sumbawanga.   
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na viungo Mbrazil, Gerson Fraga Mzambia, Clatous Chama, Luis Miquissone kutoka Msumbiji na Mzawa Muzamil Yassin.
  Fraga aliifungia bao la kwanza Simba SC kwa shuti kali dakika ya 20 akimalizia krosi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama, ambaye alifunga la pili dakika ya 49 akimalizia pasi ya Nahodha John Bocco.
  Miquissone akaifungia bao la pili Simba SC dakika ya 52  akimalizia mpira uliookolewa kwa kichwa na Nahodha wa Yanga SC, Papy Kabamba Tshishimbi baada ya krosi ya kiungo Mkenya, Francis Kahata.
  Yanga SC wakapata bao lao pekee kupitia kwa kiungo wao, Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 70 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki wa kulia, Juma Abdul.
  Kiungo Muzamil Yassin akashindilia msumari wa moto kwenye jeneza la Yanga SC kwa kufunga bao la nne dakika ya 88 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Metacha Mnata baada ya shuti la mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere.
  Baada ya mechi ninaweza kusema aliefungwa si Yanga bali kocha wa Yanga na benchi zima la ufundi sababu za kufungwa. Simba wasijifu hawakukutana na first eleven!!

  1. kwanza jana ulikosekana utatu ambao ni injini ya Yanga Mapinduzi Balama, Niyonzima na Feisal wanaomchezesha Morrisson hivyo timu ilikatika katikati na Morrison kukosa wa kumchezesha
  2. Yanga ilipaswa kumuanzisha beki Kelvin Yondan mwenye uzoefu na mechi hizi si wageni watupu  Makapu na  Lamine ambao walimfanya Nickson aonekane ni mwiba kumbe jembe la Yanga halikuwepo nyuma Yondani
  3. Kwakuwa ni mechi Simba walikamia pembeni kushoto alipaswa kukaa Adeyum kulinda na si Jafari aliepanda na kupoteza ukabaji Simba wakajinafasi kujifanya wajuaji sana wakati mechi iliyopita walikaa chini!!
  4.Deus Kaseke alipaswa kuingia sub na Sibomana fundi mwenye kasi na ari kubwa angeanza 
  5. Mbele Yanga ilikufa Sababu ya kumkosa Ditram Nchimbi huyu alipaswa kuanza na si kusubiri timu ishaaibika ndo aingie!! Molinga alionesha kuwa butu tangu mwanzo ilipaswa atolewe mapema kipindi cha kwanza kwakuwa alikuwa pia mzigo kwa kutokukaba
  6. Tshishimbi hakuwa mchezoni alipoteza mipira mingi dakika za mwanzo ilipaswa atolewe mapema aingie kiungo Mkabaji Makame mwenye ari na uchungu na timu
  7. Timu ilishafungwa kipindi cha kwanza haikupaswa kurudi yote uwanjani waliozidiwa Molinga, Lamine, Tshishimbi na Jafari hawakupaswa kurudi hili ni kosa kubwa la kocha
  8. Niyonzima pia siku haikuwa yake alipaswa kupumzika mapema aingie Ngasa
  9. Refa aliwabeba Simba ambao kila physical battle walijilegeza na kujiangusha na kumdanganya refa na pia linesman alionesha offside moja ya Yanga mwanzoni mwa mchezo kwa kuwa hakuwa akienda na move alikuwa mbele. marudio ya picha ya video yalionesha mchezaji wa Yanga hakuwa ameotea 
  10. Hatuwezi kuhitimisha bila kuitaja Simba kuivuruga Yanga kwa fitna za kumuharibu kiakili mchezaji aliewaua mara mwisho Morrisson kwa kumpa rushwa na kumshawishi kujiunga nao, huo si uanamichezo na si uungwana na ni ushamba tu huu ushindi wao hauna ladha na haujawauma wana Yanga, 
  Jana kafungwa kocha Luc kwa kupanga timu mbovu na pia kukosekana Mapinduzi pengo limeonekana
  Kocha anaweza kutuachia timu yetu kama vipi!!
  (Imeandikwa na Makusudi Lubosangija, shabiki wa Yanga Jijini Mwanza)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HAIKUFUNGWA YANGA, BALI KOCHA NA BENCHI LAKE ZIMA LA UFUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top