• HABARI MPYA

  Saturday, July 18, 2020

  SINGIDA UNITED YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-0 MLANDIZI, KMC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 1-0 GAIRO

  Na Mwandishi Wetu, MLANDIZI
  TIMU ya Singida United imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Ushindi huo uliotokana na mabao ya Seiri Arigumaho dakika ya 13 na Ramadhan Hashimu dakika ya 60 unaifanya Singida United ifikishe pointi 18 baada ya kucheza mechi 36, ingawa inaendelea kushika mkia ikiwa tayari imekwishaipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 47 baada ya mechi 36 pia. 
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, bao pekee la Ramadhani Kapera dakika ya 56 limeipa KMC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro. 


  Naye Samson Madeleke akaifungia bao pekee Mbeya City dakika ya 49 ikiwalaza wenyeji, Ndanda SC 1-0 Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
  Namungo FC ikalazimishwa sare ya  1-1 na Tanzania Prisons Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi, Edward Manyama akianza kuwafungia wenyeji dakika ya 43 kabla ya Samson Mbangula kuwasawazishia wageni dakika ya 64.
  Bao la Ayoub Lyanga dakika la 90 na ushei likainusuru Coastal Union kulala mbele ya wenyeji Biashara United waliotangulia kwa bao la kiungo mkongwe, Ramadhani Chombo ‘Redondo’ dakika ya saba timu hizo zikitoka sare ya 1-1 na Uwanja wa Karume Musoma mkoani Mara.
  Polisi Tanzania ikaibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba Bukoba. Iddy Mobby alijifunga dakika ya 18 kuipa bao la kuongoza Kagera Sugar kabla ya Sixtus Sabilo kuisawazishia Polisi dakika ya 45 kwa penalti na Marcel Kaheza kufunga la pili dakika ya 86.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-0 MLANDIZI, KMC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 1-0 GAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top