• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 05, 2020

  NIYONZIMA AUMIA MAPEMA YANGA SC YAAMBULIA SARE YA 0-0 KWA BIASHARA UNITED MUSOMA

  Na Mwandishi Wetu, MUSOMA
  YANGA SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
  Sare hiyo inayoiongezea pointi moja kila timu, inaifanya Yanga SC ifikishe pointi 61 baada ya kucheza mechi 33 na inabaki nafasi ya pili, ikiizidi pointi mbili Azam FC ambayo inamenyana na Singida United Saa 1:00 usiku leo.
  Katika mchezo wa leo, Yanga SC ilipata pigo mapema dakika ya tisa baada ya kiungo wake tegemeo, Haruna Niyonzima kuumizwa na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Abdulaziz Makame.

  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, mabingwa SImba SC wamelazimishw asare ya 0-0 pia na Ndanda SC Uwanja wa Nangwanda SIjaona Mtwara.
  Nayo Alliance FC imelazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar ya Morogoro Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza, wenyeji wakitangulia kwa bao la kujifunga la Henry Joseph dakika ya kwanza kabla ya Salum Kihimbwa kuwasawazishia wagen dakika ya 55. 
  Kikosi cha Biashara United kilikuwa; Daniel Mgore, Deogratius Mafie, Ally Kombo, Atupele Green, Novatus Miroshi, Abdulmajid Mangaro, Mpapi Salum, Mustha Batozi, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, James Mwasote na Justin Bilary.
  Yanga SC; Farouk Shikhalo, Juma Abdul, Kelvin Yondan/Mrisho Ngassa dk67, Said Juma ‘Makapu’, Lamine Moro, Adeyoum Ahmed, Feisal Salum/Tarik Kiakala dk88, Haruna Niyonzima/Abdulaziz Makame dk9, David Molinga, Deus Kaseke/Erick Kabamba dk88  na Ditram Nchimbi/Patrick Sibomana dk67.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NIYONZIMA AUMIA MAPEMA YANGA SC YAAMBULIA SARE YA 0-0 KWA BIASHARA UNITED MUSOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top