• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 19, 2020

  MEDDIE KAGERE AFUNGA MABAO MAWILI, SIMBA SC IKIISHUSHIA MBAO FC KIPIGO KIZITO TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu ya Tanzana Bara, Simba SC leo wameibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Alliance FC ya Mwanza Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.  
  Kwa ushindi huo, timu hiyo ya kocha Mbelgiji Sven-Ludwig Vandenbroeck inafikisha pointi 84 baada ya kucheza mechi 36 sasa wakiwazidi pointi 16 watani wao wa jadi, Yanga SC.
  Mabao ya Simba yamefungwa na Mnyarwanda Meddie Kagere mawili, moja kwa penalti dakika ya 24 na lingine dakika ya 44, Mmakonde wa Msumbiji Luis Miquissone dakika ya 64, Mkongo Deo Kanda dakika ya 76 na mzawa Said Ndemla dakika ya 87, wakati bao pekee la Alliance lmefungewa na Martin Kiggi dakika ya 39. 


  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, bao la dakika ya 80 ya Paul Materazi limeinusuru Lipuli FC kulala nyumbani mbele ya Azam FC iliyotangulia kwa bao la Abdallah Kheri dakka ya 44 timu hizo zikitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Samora, Iringa.
  Na JKT Tanzana ikalazimishwa sare ya 1-1 na Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, wenyeji wakitangulia kwa bao la Frank Nchimbi dakika ya 45 na ushei kabla ya Abdulkarim Segeja kuwasawazishia wageni dakika ya 57.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Benno Kakolanya, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Kennedy Juma, Pascal Wawa, Jonas Mkude/Muzamil Yassin DK46, Luis Miqussone/Hassan Dilunga dk79, Gerson Fraga ‘Viera’, Meddie Kagere, Clatous Chama/Said Ndemla dk79 na Francis Kahata/Deo Kanda dk65.
  Alliance FC; John Mwanda, Israel Patrick, Joseph James, Erick Murilo, Geoffrey Luseke, Shaaban William, David Richard/Sameer Vincent dk53, Deus Cosmass, Michael Chinedu, Juma Nyangi na Martin Kiggi/Zabona Hamisi dk80.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MEDDIE KAGERE AFUNGA MABAO MAWILI, SIMBA SC IKIISHUSHIA MBAO FC KIPIGO KIZITO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top