• HABARI MPYA

    Friday, July 03, 2020

    MAREFA WALIOCHEZESHA MECHI YA YANGA SC NA AZAM FC JUNI 21 UWANJA WA TAIFA WAFUNGIWA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    REFA Elly Sasii na wasaidizi wake, Soud Lila na Mbaraka Haule wamefungiwa miezi mitatu kwa kosa la kutokuumudu mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga SC na Azam FC uliomalizika kwa sare ya bila kufungana Juni 21, mwaka hu Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
    Maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa Vyombo vya Habari kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
    Taarifa ya Kamati hiyo maarufu kama Kamat ya Saa 72 leo imesema kwamba adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 39(1) kuhusu udhibiti wa waamuzi.
    Aidha, klabu Yanga SC imepigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la mashabiki wake kuwarushia chupa za maji wachezaji wa Namungo walipokuwa wanashangilia baada ya kufunga bao la pili Juni 23 Uwanja wa Taifa timu hizo zikitoa sare ya 2-2.
    Taarifa imesema kwamba tukio hilo lilitokea baada ya wachezaji wa Namungo FC kushangilia na kupita karibu na walipokaa washabiki wa Yanga na adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa Klabu
    Nayo Azam FC imepigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la wachezaji na maofisa wa timu hiyo kuingia uwanjani kwa kupitia lango tofauti na lililoandaliwa katika mechi ya Ligi Kuu namba 315 dhidi ya Biashara United FC iliyochezwa Juni 23.
    Taarifa  hiyo imedai kwamba Azam FC walitoa kisingizio kwamba walizuiwa kuingia kupitia mlango ulioelekezwa ingawa hakuwasaidia kuepuka adhabu iliyotolewa kwa mujibu ya kanuni ya 14(49) kuhusu taratibu za mchezo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAREFA WALIOCHEZESHA MECHI YA YANGA SC NA AZAM FC JUNI 21 UWANJA WA TAIFA WAFUNGIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top