• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 30, 2020

  AWESU AWESU ALIYEKUWA ANATAKIWA NA YANGA ASAINI MIAKA MIWILI KUJIUNGA NA AZAM FC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imekamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wa Kagera Sugar, Awesu Awesu, kwa mkataba wa miaka miwili.
  Awesu ambaye alikuwa anawaniwa pia na vigogo, Yanga SC, anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Azam FC kwenye dirisha kubwa la usajili kwa ajili ya msimu ujao, ukiwa ni usajili huru baada ya kumaliza mkataba wake Kagera Sugar.
  Kiungo huyo ambaye aliwahi kulelewa kwenye kituo cha Azam Academy kwa miaka miwili 2014-2015, amesaini mkataba huo leo Alhamisi jioni mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'.
  Rasta huyo amekuwa na kiwango kizuri kwa misimu miwili mfululizo akiwa na Singida United na msimu huu Kagera Sugar, katika mashindano yote msimu huu akiwa amefunga jumla ya mabao saba.
  Imemchukua safari ya miaka mitano kwa Awesu kurejea tena Azam FC, baada ya kuondoka Azam Academy mwaka 2015, akijiunga na Madini ya Arusha, kabla ya kutua Mwadui kisha Singida United na msimu uliopita Kagera Sugar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AWESU AWESU ALIYEKUWA ANATAKIWA NA YANGA ASAINI MIAKA MIWILI KUJIUNGA NA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top