• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 30, 2020

  MAREFA WATANO KUCHEZESHA FAINALI YA AZAM SPORTS FEDERATION CUP SUMBAWANGA JUMAPILI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kwa pamoja na Bodi ya Ligi wametaja marefa watakaochezesha Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) Jumapili Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Hao ni Abubakar Mturo wa Mtwara, Abdallah Mwinyimkuu wa Singida, Ahmed Arajiga wa Mara, Ramadhani Kayoko wa Dar es Salaam na wasaidizi wao Abdulaziz Ally wa Arusha na Hamdani Said wa Mtwara.  
  Wote hao watakuwa chini ya mkufunzi Israel Mujuni Nkongo, Mtathmini wa Mechi Soud Abdi wa Arusha na Kamisaa Omar Gindi wa Kigoma.
  Tayari kikosi cha Namungo FC kipo Sumbawanga tangu jana kwa ajili ya kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya Lindi kutwaa taji hilo, wakati Simba SC wao siku mbili hizi nao watasafiri kwenda Sumbawanga.
  Azam Sports Federation Cup (ASFC) ni michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania ambayo bingwa wake hushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Lakini kwa mwaka huu Namungo imejihakikishia kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani hata kama itafungwa, kwani tayari Simba SC ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo na 21 jumla ambao watacheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAREFA WATANO KUCHEZESHA FAINALI YA AZAM SPORTS FEDERATION CUP SUMBAWANGA JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top