• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 21, 2018

  SIMBA NA YANGA ZA MAREKANI KUMENYANA JULAI 7, MONALISA AJA KUNOGESHA MAMBO

  Na Mahmoud Zubeiry, NEW YORK
  KUTAKUWA na mchezo wa soka kati ya wapenzi wa Simba na wapenzi wa Yanga miongoni mwa Watanzania waishio nchini Marekani Julai 7, mwaka huu hapa mjini Washington DC.
  Hiyo itakuwa katika sehemu ya tamasha la kila mwaka la DMV Old School Reunion litakaloanza Julai 6 likifanyika maeneo tofauti.
  Mechi itaanza Saa 10:00 jioni kwa saa za Marekani na itafanyika Uwanja wa 830 Ridge Rd, SE Washington, DC 20019 na rekodi inaonyesha wapenzi wa Yanga wamekuwa wakiitambia Yanga.

  Aliyekuwa mkuu wa utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lilly Munanka akisalimiana na wachezaji wa Yanga ambao ndio walichukua kombe la DICOTA mwaka 2011 mjini Washington 

  Nyota wa Bongo Muvi, Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ ni miongoni mastaa ambao wanatarajiwa kupambana burudani hizo ambazo zitapambwa na starehe, vyakula, vinywaji, Fasheni, Michezo na Nyama choma.
  Ijumaa ya Julai 6 hadi 8 mambo yatakuwa Oxford Center, 9700 Martin L King Jr Hwy, Lanham, MD 20706 kabla ya kumalizia kwa disko la nguvu kuanzia Saa 3:00 usiku DMV International VIBE kwa kiingilio cha dola 50 ambacho kitaambatana na pfa ya kinywaji.
  Jumamosi ya July 7 kuaniza Saa 4:00 asubuhi litafanyika Bonanza la Basketball viwanja vya 830 Ridge Rd, SE mjini Washington, DC 20019 kabla ya mchezo wa Simba na Yanga kuchukua nafasi 830 Ridge Rd, SE mjini Washington, DC 20019.
  Na kuanzia Saa 3:00 usiku litaporomoshwa disko la nguvu la “Old School Reunion Party” ambalo halijawabui kutokea chini ya ma DJ wakali Amerika Kaskazini,. Dj Luke Joe na Dj Dennis The Funkhouse na siku mambo yote gharama yake itakuwa dola 80 pamoja na chakula na vinywaji kutwa kucha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA ZA MAREKANI KUMENYANA JULAI 7, MONALISA AJA KUNOGESHA MAMBO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top