• HABARI MPYA

    Thursday, June 14, 2018

    SIMBA NA PRISONS, NAZO ZATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA UHAI

    Na Mwandishi Wetu, DODOMA
    SIMBA SC imefanikiwa kufuzu Robo Fainali michuano ya Ligi Kuu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, maarufu kama Kombe la Uhai inayoshirikisha vikosi vya pili vya klabu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara pamoja na kulazimishwa sare ya bila kufungana na Stand United katika mchezo wa Kundi B leo viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
    Matokeo hayo yanamaanisha Simba SC inamaliza nafasi ya pili kwenye Kundi B kwa pointi zake nne, nyuna ya vinara Stand United waliomaliza na pointi saba.

    Juma Rashid wa Simba akimtoka beki wa Stand United leo Uwanja wa UDOM

    Mechi nyingine ya kundi hilo leo, Singida United imeichapa Njombe Mji FC mabao 3-1 mabao yake yakifungwa na Emmanuel Simon mawili dakika za 27 na 52 na Ramadhani Salum dakika ya 42 dhidi ya moja la Nickson Kibabage dakika ya 57.
    Lakini pamoja na ushindi huo, Singida United inamaliza na pointi tatu za Njombe Mji FC na zote zinakwenda nje ya michuano.   
    Mechi nyingine za leo zilikuwa za Kundi D, ambako Tanzania Prisons imeichapa 5-0 Kagera Sugar mabao ya Ramadhani Ibata matatu dakika za 19, 45 na 57, Abubakar Malika dakika ya 81 na Isaac Kuwayawaya dakika ya 85 na Lipuli imatoka sare ya 1-1 na Ndanda FC.
    Tanzania Prisons imemaliza na pointi tisa baada ya kushinda mechi zake zote tatu ikiongoza  Kundi D ikifuatiwa na Ndanda FC iliyomaliza na pointi nne na zote zinaungana na Simba, Stand United, Mtibwa Sugar, Azam FC, Mbao FC na Ruvu Shooting kwenda Nane Bora.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA PRISONS, NAZO ZATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA UHAI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top