• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 22, 2018

  MTIBWA SUGAR MABINGWA KOMBE LA UHAI 2018…SIMBA SC WAIBWAGA KWA MATUTA AZAM NAFASI YA TATU

  Na Sada Salmin, DODOMA
  TIMU ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Ligi Kuu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, maarufu kama Kombe la Uhai inayoshirikisha vikosi vya pili vya klabu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand United ya Shinyanga viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Alhamisi.
  Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, Richard William dakika ya 86 na sasa timu hiyo ya Manungu mkoani Morogoro inarithi taji lililoachwa wazi na Simba SC. 
  Na ni Mtibwa Sugar hao hao waliowavua ubingwa Simba SC katika mchezo wa Nusu Fainali wakiwachapa 1-0 pia, bao pekee la Abuu Yohana dakika ya 117.

  Juni 2, mwaka huu Mtibwa Sugar ilitwaa taji la ASFC kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Singida United Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha

  Stand wao waliingia fainali baada ya kuwafunga washindi wa pili wa mwaka jana, Azam FC 1-0, bao pekee la Maurice Mahela dakika ya 32.
  Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Alhamisi, Simba SC walishinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 na Azam FC. Simba SC walitangulia kwa bao la Yahya Mbegu dakika ya saba, kabla ya Paul Peter kuisawazishia Azam FC dakika ya 33, hivyo kuiachia mikwaju ya penalti ichague mshindi wa Medali za Shaba Kombe la Uhai 2018.  
  Na huu mundelezo wa msimu mzuri kwa Mtibwa Sugar, baada ya wakubwa zao, kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) wakiichapa 3-2 Singida United katika fainali Juni 2 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR MABINGWA KOMBE LA UHAI 2018…SIMBA SC WAIBWAGA KWA MATUTA AZAM NAFASI YA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top