• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 23, 2018

  LUKAKU AFUNGA MAWILI UBELGIJI IKIITANDIKA 5-2 TUNISIA

  Mshambuliaji Romelu Lukaku akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Ubelgiji dakika za 16 na 45 na ushei katika ushindi wa 5-2 dhidi ya Tunisia leo Uwanja wa Otkrytiye Arena mjini Moscow, Urusi katika mchezo wa Kundi G Kombe la Dunia. Mabao mengine ya Ubelgiji yamefungwa na Eden Hazard mawili pia, moja kwa penalti dakika ya sita na lingine na dakika ya 51 kabla ya Michy Batshuayi kufunga la tano dakika ya 90, wakati ya Tunisia yamefungwa na Dylan Bronn dakika ta 18 na Wahbi Khazri dakika ya 90 na ushei maana yake wawakilishi wa Afrika wanatolewa baada ya kufungwa mechi mbili za mwanzo 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LUKAKU AFUNGA MAWILI UBELGIJI IKIITANDIKA 5-2 TUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top