• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 22, 2018

  MTIBWA SUGAR YAMSAJILI NYOTA WA KAGERA SUGAR MIAKA MIWILI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imeanza kujiimarisha kuelekea msimu ujao wa michuano ya Afrika, baada ya kumsajili mshambuliaji Jaffar Salum Kibaya kutoka Kagera Sugar.
  Kibaya amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga tena na timu hiyo ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro ambayo aliichezea kabla ya kwenda Kagera.
  Katibu Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabur ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba huo unakuwa usajili wa kwanza kwa timu hiyo baada ya dirisha kufunguliwa Juni 15, mwaka huu. 
  Mshambuliaji Jaffar Salum Kibaya kutoka Kagera Sugar amerejea Mtibwa Sugar kwa miaka miwili

  “Kibaya ni mchezaji ambaye anarejea nyumbani, kwa sababu kama utakumbuka tulikuwa naye hapa kabla hajakwenda Kagera Sugar,”amesema Swabur.
  Mtibwa Sugar itaiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya kufanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Juni 2, mwaka huu kwa ushindi wa mabao 3-2 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAMSAJILI NYOTA WA KAGERA SUGAR MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top