• HABARI MPYA

  Tuesday, June 26, 2018

  ROJO AIPELEKA ARGENTINA 16 BORA, KUIVAA UFARANSA

  Beki Marcos Rojo akikimbia kushangilia kishujaa huku amedandiwa mgongoni na Nahodha wake, Lionel Messi baada ya kuifungia Argentina bao la ushindi dakika ya 86 ikiilaza Nigeria 2-1 katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Dunia leo Uwanja wa Saint-Petersburg nchini Urusi. Argentina ilitangulia kwa bao la Messi dakika ya 14, kabla ya Victor Moses kuisawazishia Super Eagles kwa penalti dakika ya 51, kufuatia Javier Mascherano kumshika hadi kumungusha Leon Balogun kwenye boksi wakati wa kona. Lakini refa Cuneyt Cakir aliingia lawamani kwa kuwanyima penalti ya pili Nigeria, huku Argentina ikienda hatua ya 16 Bora kama mshindi wa pili wa kundi kwa pinti zake nne nyuma ya Croatia, iliyomaliza na pointi tisa. Argentina itamenyana na Ufaransa Juni 30, wakati Croatia itamenyana na Denmark Julai 1 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROJO AIPELEKA ARGENTINA 16 BORA, KUIVAA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top