• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 21, 2018

  MSHAMBULIAJI MPYA AZAM AAHIDI KUIPIGANIA TIMU IFANYE VIZURI, MWAMBUSI NAYE...

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI mpya wa Azam FC, Ditram Nchimbi ameanza kujifua na timu hiyo na moja kwa moja amesema atapambana kuhakikisha anafanya vizuri katika kikosi cha timu hiyo.
  Nchimbi amejiunga na Azam FC katika siku za hivi karibuni akitokea Njombe Mji ambayo imeshuka daraja katika Ligi Kuu ya Vodacom.
  Akizungumza katika mazoezi ya timu hiyo, Nchimbi amesema anashukuru amepokelewa vizuri na wachezaji wenzake katika kikosi cha timu hiyo tangu alipojiunga nao siku chache zilizopita.

  Ditram Nchimbi amesema atapambana kuhakikisha anafanya vizuri Azam FC

  “Wenzangu wamenipokea vizuri, kazi niliyonayo sasa ni kuhakikisha napambana ipasavyo kuweza kuisaidia timu katika kuifikisha katika mafanikio.
  “Nitajituma kwa muda wote na kupambana kwa kushirikiana na wenzangu ili timu iweze kufika mbali,” alisema Nchimbi aliyewahi kutamba na Mbeya City.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSHAMBULIAJI MPYA AZAM AAHIDI KUIPIGANIA TIMU IFANYE VIZURI, MWAMBUSI NAYE... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top