• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 27, 2018

  KOREA KUSINI YAIVUA UJERUMANI UBINGWA WA DUNIA

  UJERUMANI imevuliwa ubingwa wa dunia baada ya kufungwa mabao 2-0 na Korea Kusini leo katika mchezo wa Kundi F Kombe la Dunia Uwanja wa Kazan Arena nchini Urusi.
  Mabao yaliyoizamisha Ujerumani waliobeba taji hilo mwaka 2014 nchini Brazil kwa kuifunga Argentina 1-0 katika fainali yamefungwa na Kim Young-Gwon dakika ya 90 (ongeza mbili za majeruhi) na Son Heung-Min dakika ya 90 ( (ongeza sita za majeruhi).
  Ujerumani inatolewa mashindanoni baada ya kuambulia pointi tatu tu kutokana na ushindi wa 2-1 dhidi ya Saudi Arabia na kupoteza mechi mbili, kwani kabla ya leo walifungwa 1-0 na Mexico inayoungana na Sweden kwenda hatua ya 16 Bora.
  Korea Kusini pamoja na ushindi wa leo imeaga pia mashindano, kwani imemaliza na pointi tatu sawa na Ujerumani ya kocha Joachim Low .
  Hii ni mara ya kwanza ndani ya miaka 80 kwa Ujeruman kutolewa katika hatua ya makundi ya kombe la Dunia. Nayo Sweden imeichapa 3-0 Mexico, mabao ya Ludwig Augustinsson dakika ya  50, Andreas Granqvist kwa penalti dakika ya 62 na Edson Álvarez aliyejifunga dakika ya 74.  

  Timo Werner wa Ujerumani akisikitika baada ya kupoteza nafasi nzuri ya kuwafunga Korea Kusini 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOREA KUSINI YAIVUA UJERUMANI UBINGWA WA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top