• HABARI MPYA

  Monday, June 18, 2018

  CROATIA YAMTIMUA STRAIKA ALIYEGOMA KUINGIA UWANJANI

  STRAIKA wa Croatia, Nikola Kalinic amerudishwa nyumbani kutoka nchini Urusi baada ya kugoma kuingia uwanjani katika mchezo wa Kombe la Dunia wa nchi yake dhidi ya Nigeria ambapo walishinda mabao 2-0.
  Kalinic alianzia benchi katika mchezo huo lakini zikiwa zimebaki dakika tano mchezo huo kuisha, Kocha wa Croatia, Zlatko Dalic alimtaka straika huyo kujiandaa kuingia kuchukua nafasi Mario Mandzukic. 
  Hata hivyo, habari zaidi zinasema mshambuliaji huyo amelalamika kutimuliwa kwake kunausiana na mambo mengine tofauti na mzozo wa yeye kukataa kuingia kuchukua nafasi ya Mandzukic.

  Kocha wa Croatia alilazimika kumuingiza Marko Pjaca badala ya Kalinic, ambaye kiuhalisia ni mshambuliaji wa pembeni lakini akachezeshwa kama straika.
  Kocha Dalic hakulidhishwa na kitendo cha kugomewa na Kalinic na alionyesha wazi kukasirika kutokana na nidhamu hiyo ya mchezaji wake.
  Uamuzi huo wa kumuondoa kikosini straika huyo wa AC Milan umefikiwa leo Jumatatu asubuhi na Kalinic ataondoka muda wowote kuanzia sasa.
  Kitendo cha kuondolewa kikosini kwa Kalinic, kunaifanya Croatia kubaki na straika mmoja tu ambaye ni Mandzukic.
  Baadaye leo Kocha wa Croatia Dalic atazungumza na waandishi wa habari kufafanua kilichotokea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CROATIA YAMTIMUA STRAIKA ALIYEGOMA KUINGIA UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top