• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 29, 2018

  LIPULI YAWAONGEZEA MIKATABA NYOTA WAKE WANNE KUELEKEA MSIMU UJAO

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA
  TIMU ya Lipuli ya Iringa imewasainisha mikataba mipya wachezaji wake wanne ili kuwaweka mbali na klabu zinazowatamani kwa sasa.
  Wakati dirisha la usajili likiwa wazi tangu Juni 15, uongozi wa Lipuli umerudi nyuma na kutazama usalama wa wachezaji wake.
  Na Alhamisi Lipuli imewasainisha mikataba mipya wachezaji wake wane, beki Emmanuel Kichiba, viungo Shaabani Ada, Yussuf Mohamed na mshambuliaji, Malimi Busungu. 


  Shaabani Ada (kushoto) akikabidhiwa mkataba wake mpya baada ya kusaini leo mjini Iringa 

  Na Lipuli inachukua hatua hiyo ikiwa katika maandalizi ya mwanzo kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ambao utakuwa wa pili tangu ipande tena baada ya miaka mingi. 
  Wachezaji wote walioongezewa mikataba ni muhimu na hatua hiyo imekuja baada ya pendekezo la kocha Mkuu, Suleiman Matola ambye aliagiza watiwe pingu mapema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIPULI YAWAONGEZEA MIKATABA NYOTA WAKE WANNE KUELEKEA MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top