• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 17, 2018

  SINGIDA UNITED YASAJILI MKALI MWINGINE WA TANZANIA PRISONS, NI MSHAMBULIAJI ELIUTER MPEPO

  Na Mwandishi Wetu, SINGIDA
  TIMU ya Singida United imeendelea kujiimarisha kwa kumsajili mshambuliaji chipukizi wa Tanzania Prisons, Eleuter Herman Mpepo kwa mkataba wa miaka miwili.
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo pamoja na kumtambulisha mchezaji huyo, lakini pia amesema kwamba wana matumaini makubwa na mchezaji huyo.
  “Mpepo anazimudu vyema nafasi zote za ushambuliaji na amesajiliwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na maafande hao wa Jeshi la Magereza,” amesema.
  Mpepo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa Singida United kutoka Tanzania Prisons, baada ya kiungo Kazungu Mashauri aliyesajiliwa mwezi uliopita.
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo akimkabidhi jezi ya timu hiyo Eliuter Mpepo 

  Eliuter Mpepo akiwa na jezi ya Singida United baada ya kusaini

  Na kwa ujumla, Mpepo anakuwa mchezaji wa saba kusajiliwa Singida United kuelekea msimu ujao, wengine Daniel Lyanga kutoka Fanja ya Oman, Tibar John kutoka Ndanda FC, Habib Kiyombo kutoka Mbao FC, Mbrazil Felipe Oliveira na Muivory Coast, Diaby Amara.
  Ikumbukwe msimu ujao Singida United msimu ujao itakuwa chini ya kocha mpya, Hemed Morocco baada ya kuachana na Mholanzi, Hans van der Pluijm aliyehamia Azam FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED YASAJILI MKALI MWINGINE WA TANZANIA PRISONS, NI MSHAMBULIAJI ELIUTER MPEPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top