• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 29, 2018

  SERIKALI YAENDELEA NA UKARABATI WA VIWANJA KUELEKEA FAINALI ZA AFCON U17 MWAKANI

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  SERIKALI kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea na maandalizi yanakayohusisha ukarabati wa miundombinu ya viwanja vitakavyotumika kwa michuano ya soka ya mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON-U17).
  Michuano hiyo ya kimataifa ndiyo ya kwanza kufanyika nchini, timu ya vijana ya Tanzania Bara 'Serengeti Boys' ipo kambini ikiendelea kujifua.

  Waziri Mkuu, Dk. Kassim Majaliwa, amesema kwamba michuano ya U17 ni fursa nzuri kufanika Tanzania 

  Katika hotuba yake bungeni jijini Dodoma leo kuahirisha mkutano wa 11 wa Bunge la 11, Waziri Mkuu, Dk. Kassim Majaliwa, amesema kwamba michuano hiyo ni fursa nyingine ya kipekee ya kutangaza Tanzania katika nyanja za kimataifa. 
  "Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea na maandalizi stahiki ambayo yatahusisha pia ukarabati wa miundombinu ya viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo," amesema.
  Kiongozi huyo wa serikali ametoa wito kwa wananchi kutumia vizuri uwapo wa mashindano hayo kujiongezea kipato kupitia biashara ya bidhaa na huduma kwa wageni. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SERIKALI YAENDELEA NA UKARABATI WA VIWANJA KUELEKEA FAINALI ZA AFCON U17 MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top