• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 21, 2018

  DENMARK KUMKOSA PAULSEN MECHI NA UFARANSA

  TIMU ya taifa ya Denmark itamkosa mshambuliaji wake mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi C dhidi ya Ufaransa baada ya leo kuonyeshwa kadi ya pili ya njano katika sare ya 1-1 na Australia Uwanja wa Samara Arena, Urusi.
  Yussuf alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Antonio Mateu raia wa Hispania katika dakika ya 37 kabla ya kutolewa na Kocha Aage Hareide dakika ya 59 na nafasi yake akaingia Martin Braithwaite.
  Katika mchezo huo, bao la Denmark lilifungwa na Christian Eriksen anayechezea Klabu ya Tottenham Hotspur ya England katika dakika ya saba.

  Refa Mspaniola, Antonio Mateu (katikati) akimuonyesha kadi ya njano Yussuf Poulsen (kulia) leo  

  Australia ilisawazisha kwa njia ya penalti katika ya 38 mfungaji akiwa ni Mile Jedinak. Penalti hiyo ilipatikana baada ya Yussuf kuushika mpira katika eneo la hatari.
  Hii ni penalti ya pili inasababishwa na Yussuf katika lango la Denmark kwani katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Peru, mchezaji huyo mwenye asili ya Tanzania alisababisha penalti ambayo haikuzaa bao.
  Denmark sasa inaongoza Kundi C ikiwa na pointi nne baada ya kuifunga Peru bao 1-0 katika mchezo wa kwanza huku Ufaransa ambayo saa 12:00 jioni ya leo itacheza na Peru katika mchezo mwingine wa Kundi C.
  Denmark itacheza mchezo mwingine Jumanne ya Juni 26, mwaka huu dhidi ya Ufaransa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DENMARK KUMKOSA PAULSEN MECHI NA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top