• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 27, 2018

  SAMPAOLI ALIMUOMBA RUHUSA MESSI KUMUINGIZA AGUERO

  KOCHA wa Argentina, Jorge Sampaoli jana alimuomba ruhusa Nahodha, Lionel Messi kumuingiza mshambuliaji Sergio Aguero dakika za mwishoni katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Dunia dhidi ya Nigeria.
  Bao la dakika ya 86 la Marcos Rojo lilipa ushindi wa 2-1 Nigeria, mabingwa mara mbili wa Kombe la Dunia na kufuzu hatua ya 16 Bora ya michuano ya mwaka huu nchini Urusi.
  Lakini Argentina ilijikuta katika wakati mgumu mbele ya wawakilishi wa Afrika Uwanja wa St Petersburg baada ya kunabwa kwa sare ya 1-1 hadi dakika ya 85 na kukaribia kutolewa hatua ya makundi.
  Na ndipo Sampaoli alipomtuma mmoja wa wasaidizi wake kwenda kuomba ruhusa kwa Messi amuingize Aguero. 
  Jorge Sampaoli aliomba ruhusa kwa Lionel Messi kumuingiza Sergio Aguero dakika za mwishoni jana dhidi ya Nigeria 

  Baada ya nyota mkubwa wa timu, Messi kuzungumza na msaidizi huyo pembezoni mwa Uwanja karibu na benchi, Sampaoli akasikika akiuliza: "Flea, nifanyeje? Nimuingize Kun?'
  Messi alitoa ruhusa na kurejea uwanjani na mshambuliaji huyo wa Manchester City akaingizwa kuchukua nafasi ya beki Nicolas Tagliafico zikiwa zimebaki dakika 10 kabla ya beki wa Manchester United, Rojo kufunga la ushindi dakika sita baadaye.
  Tukio hilo ni muendelezo wa matukio yanayozidi kumshushia imani kocha huyo kwenye kikosi cha Argentina tangu wawasili Urusi mapema mwezi huu.
  Argentina ilifanya mkutano na Waandishi wa Habari bila kocha huyo Jumapili huku kukiwa na habari kwamba wachezaji wakubwa kama Messi na Javier Mascherano wamepoteza imani naye. 
  Mtendaji Mkuu wa FA, Claudio Tapia alikanusha madai hayo na kwamba Sampaoli atafukuzwa wakati wowote, huku Mascherano akikiri kwamba wachezaji waandamizi waliwafuata viongozi wa FA Ijumaa usiku kuzungumzia mambo ya kiufundi.
  Ilifikiriwa kwamba kikosi cha Argentina kimepoteza imani kwa Sampaoli kwa kuchezesha mabekki watatu katika kipigo cha 3-0 kutioka kwa Croatia wiki iliyopita. 
  Jana walitumia mfumo wa 4-3-3 ili kumpa nafasi zaidi Messi na kwenye kikao hicho ilielezwa wazi kwamba wamepoteza imani na kocha huyo wa zamani wa Chile na Sevilla.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMPAOLI ALIMUOMBA RUHUSA MESSI KUMUINGIZA AGUERO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top