• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 27, 2018

  KOCHA MBEYA CITY KUSAJILI WAKALI WATANO KUTOKA BURUNDI KUIMARISHA KIKOSI TIMU ITISHE MSIMU UJAO

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa Mbeya City, Ramadhani Nsanzurwimo amesema kwamba yupo katika mchakato wa kuangalia wachezaji aliowapendekeza nchini Burundi kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha timu hiyo kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online kwa simu jana kutoka kwao, Burundi kocha huyo alisema alipendekeza nafasi tatu za kusajili Warundi watano ambao ni beki mmoja wa kati, viungo wawili pamoja na washambuliaji wawili wanaojua kufunga.
  Alisema kipindi ambacho yupo Burundi katika mapumziko ataangalia uwezekano wa kupata mchezaji anayemuhitaji atakayesaidia timu hiyo kwa msimu ujao.

  Kocha wa Mbeya City, Ramadhani Nsanzurwimo anataka kusajili nyota watano kutoka Burundi 

  "Nikipata mchezaji nitashauriana na uongozi ili kumsajili, tunahitaji maboresho ndani ya kikosi cha Mbeya hivyo muhimu kusajili wachezaji watakaotuletea matokeo mazuri," alisema.
  Nsanzurwimo alisema pamoja na Burundi mpango wa kusajili wachezaji wazawa wa Tanzania kuimarisha zaidi kikosi unaendelea baada ya kuuachia uongozi mapendekezo yake.
  Kocha huyo akizungumzia juu ya kuongeza mkataba mwingine alisema ana matarajio makubwa ya kurejea kukinoa kikosi cha timu hiyo.
  "Nimezungumza na viongozi wa Mbeya wameniambia bado wanahitaji kuendelea nao, hivyo muda wowote nitarejea Tanzania kwa ajili ya mazungumzo Rasmussen," alisema.
  Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe amesema kwamba watamuongezea mkataba kocha huyo Julai Mosi na baada ya hapo wataanza usajili wa wachezaji wapya kwa lengo la kuongeza nguvu ndani ya timu hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA MBEYA CITY KUSAJILI WAKALI WATANO KUTOKA BURUNDI KUIMARISHA KIKOSI TIMU ITISHE MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top