• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 25, 2018

  MISRI YAPIGWA TENA NA KUTOLEWA KINYONGE KOMBE LA DUNIA

  Mohamed Salah akiifungia Misri bao la kwanza dakika ya 22 wakifungwa mabao 2-1 na Saudi Arabia katika mchezo wa Kundi A Kombe la Dunia Uwanja wa Volgograd Arena nchini Urusi na kutolewa kwenye michuano hiyo waliyokuwa wakishiriki kwa mara ya kwanza tangu 1990. Hiyo ni baada ya kufungwa 1-0 na Uruguay Juni 15 na 3-1 na Urusi Juni 19 katika mechi zake mbili za kwanza. Mabao ya Saudi Arabia iliyopata ushindi wa kwanza Kombe la Dunia tangu mwaka 1994 yamefungwa na Salman Al Faraj kwa penalti dakika ya 45 na ushei na Salem Al Dawsari dakika ya 90 na ushei 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MISRI YAPIGWA TENA NA KUTOLEWA KINYONGE KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top