• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 27, 2018

  DAKADAHA YA SOMALIA, PORTS YA DJIBOUTI NA KATOR YA SUDAN KUSINI ZATUA DAR KWA KOMBE LA KAGAME

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU za soka za Dakadaha ya Somalia, Ports ya Djibouti na Kator FC ya Sudani Kusini zimekuwa timu za kwanza kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa michuano ya Kombe La Kagame.
  Michuano ya Kombe la Kagame inayozijumuhisha timu za Afrika Mashariki na Kati inaandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
  Wachezaji wa Klabu ya Dakadaha ya Somalia muda mfupi baada ya kuwasili nchini wamesema wanaiogopa Simba tu katika michuano hiyo na wana uhakika wa kufanya vizuri.
  “Tumekuja kupambana kwa ajili ya klabu na nchi yetu na tumejiandaa kufanya vizuri,” alisema Abdulmajid Athuman.
  Kikosi cha Dakadaha ya Somalia ambacho tayari kimewasili Dar es Salaam tayari kwa michuano ya Kagame

  “Timu nyingi katika michuano hii tunaziona ni timu za kawaida ila tunaijua Simba ya Tanzania ndiyo timu kali hivyo tunayoihofia kukutana nayo maana tupo nayo kundi moja,” Kasolo Mustapha.
  CECAFA imezitaka klabu hizo za Dakadaha, Ports na Kator FC kujisikia zipo salama katika ardhi ya Tanzania kwa muda wote zitakaoshiriki michuano hiyo.
  Dakadaha imefikia katika Hoteli ya Saphire, Ports wenyewe wapo Hoteli ya Rungwe na Kator FC ipo kwenye Hoteli ya Spice.
  Michuano hiyo ya Kombe la Kagame itaanza rasmi Ijumaa wiki hii kwenye viwanja vya Taifa na Azam Complex.
  Mechi za kwanza siku hiyo kwenye Uwanja wa Azam Complex, JKU ya Zanzibar itaanza kucheza na Vipers ya Uganda saa nane halafu saa kumi jioni uwanjani hapo mabingwa watetezi Azam FC watacheza na Kator.
  Saa moja kamili usiku kwenye Uwanja wa Taifa, Singida United itacheza na APR ya Rwanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DAKADAHA YA SOMALIA, PORTS YA DJIBOUTI NA KATOR YA SUDAN KUSINI ZATUA DAR KWA KOMBE LA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top