• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 19, 2018

  TFF YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA LA LIGA KWA MIAKA MITATU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa miaka mitatu na Ligi kuu ya nchini Hipania (LA LIGA) kwaajili ya kuendeleza mpira wa miguu nchini Tanzania. 
  Hafla ya utiaji saini huo ilifanyika jana, Juni 18 mwaka huu makao makuu ya LA LIGA mjini Madrid Hispania iliyohudhuliwa name Rais wa Laliga Javier Tebas, Mkurugenz wa Maendeleo ya kimataifa wa Laliga Oscar Mayo, muwakilishi wa Laliga Tanzania Sami Hanane, Rais wa TFF Walles Karia na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura.
  Akizungumza na waandishi wa Habari leo kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF, Afisa Habari wa shirikisho hilo, Clifford Mario Ndimbo amesema kwamba hii ni hatua nyingine kwa La Liga kujikita kwenye mpira wa miguu duniani na nia yake ya kushirikiana na Taasisi mbalimbali za maeneo mbalimbali. 

  Ndimbo ameongeza kuwa kupitia makubaliano hayo Laliga itaiongoza TFF katika kuiongoza katika mchakato wa kutengeneza Ligi inayojitegemea.
  Pamoja na hayo LaLiga kwa kushirikiana na TFF watashirikiana kuandaa semina mbalimbali za ukocha, uongozi, uamuzi pamoja na semina za maendeleo ya soka la Vijana na wanawake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA LA LIGA KWA MIAKA MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top